Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA JOHANNESBURG

Rais wa kwanza mwafrika kuingoza Afrika ya kusini na mpinga ubaguzi Nelson Mandela amefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Mandela aliiongoza Afrika ya kusini kutoka katika utawala wa watu weupe na kuwa chini ya utawala wa waafrika katika miaka ya 90 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kwasababu za kisiasa.
Alikuwa akipata matibabu ya uangaizi wa hali ya juu nyumbani baada ya kukaa hospitali kwa muda wa miezi 3.
Akitangaza kupitia luninga ya Taifa Rais Jaco Zuma alisema Mandela yuko katika amani. 'Our nation has lost its greatest son'' Alisema Zuma.
"Although we knew that this day would come, nothing can diminish our sense of a profound and enduring loss." Aliongeza rais Zuma.


Mandela anaejulikana kama Madiba kwa jina la ukoo wake alifariki jijini Johannesburg.




Marehemu Nelson Mandela aliekuwa Rais wa kwanza mweusi kuingoza Afrika ya kusini akiwa ameshikilia kombe la dunia wakati mashindano ya mpira ya kombe la dunia yalipofanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika mwaka 2010.

Nelson Mandela
1918 Born in the Eastern Cape
1943 Joined African National Congress
1956 Charged with high treason, but charges dropped after a four-year trial
1962 Arrested, convicted of incitement and leaving country without a passport, sentenced to five years in prison
1964 Charged with sabotage, sentenced to life
1990 Freed from prison
1993 Wins Nobel Peace Prize
1994 Elected first black president
1999 Steps down as leader
2001 Diagnosed with prostate cancer
2004 Retires from public life
2005 Announces his son has died of an HIV/Aids-related illness

 
Mandela enzi za ujana wake.

 Woman outside Mandela's home in Johannesburg (5 Dec 2013)
Bibi akiomboleza kwa machozi nje ya nyumba ya Mandela jijini Johannesburg ambapo melfu ya waombolezaji walijaa nje ya nyumba.

Lungi Morrison, granddaughter of Archbishop Desmond Tutu, at a memorial in London (6 Dec 2013)
Jijini London Uingereza muombolezaji akiweka shada la maua nje ya ubalozi wa Afrika ya kusini.

UN Security Council
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limesimama kwa dakika moja jijini New York kuomboleza kifo cha Nelson Mandela.


Muombolezaji akiwasha moto kwenye karatasi la kupaa katika mgahawa uliopewa jina la Madiba katika kumuenzi Nelon Mandela aliefariki dunia 5/Dec/2013 huko Brooklyn borough of New York,


 
Wananchi wakiomboleza Nje ya nyumba ya zamani ya Mandela jijini Soweto ambapo sasa ni jumba la makumbusho.


Muombolezaji akiimba nje ya nyumba ya Mandela jijini Johannesburg.



Victoria Johnson na binti yake Dawn Stephens wakiomboleza nyumbani kwa Mandela


Muombolezaji akiwasha mshumaa nje ya ubalozi wa Afrika Ya Kusini uliopo jijini London.


Keaton Anderson akipigwa picha na baba yake kwenye sanamu ya Mandela nje ya ubalozi wa Afrika Ya Kusini jijini Washington,kama kumbukumbu ya kifo cha Mandela


Msanii wa uchoraji ajulikanae kwa jina la ''Franco the Great'' akiwa ameweka pozi mbele ya picha ya Mandela aliyoichora mwaka 1995 na baadae akaongezea ya Rais wa Marekani Barrack Obama katika mtaa wa 125th Harlem street uliopo karibu na New York.




Marc Easton akimsalimia Denis Du Preez mzaliwa wa Arika ya kusini na meneja wa mgahawa wa kiafrika ya kusini wa Madiba uliopo Brooklyn New York.


Michille Andrews kutoka Cape Town afrika ya kusini akimkumbatia rafiki nje ya mgahawa wa Madiba jijini New York Huku akisema haya "You don't expect it to affect you like that," akizungumzia kifo cha Mandela Nelson Mandela. "What stood out for me is that he forgave the prison guards and moved forward."

 
Waombolezaji jijini New York katika ukumbi wa starehe wa Apollo.


Watu wakiangalia mchoro wa Msanii wa Brazil Muralist Eduardo Kobra ukionesha sura ya Mandela huko jijini Los Angeles,wilaya ya Hollywood maeneo ya Highland Avenue.


No comments:

Post a Comment